NA CHRISPIN B. KALINGA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wote kuendelea kutunza mazingira na kuhifadhi vyanzo vya maji, ili kuimarisha hali ya upatikanaji wa maji na viumbe hai kwa uchumi wa Taifa.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo Aprili 01, 2023 mkoani Mtwara wakati akizindua rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru ambazo zitahitimishwa Oktoba 14 mwaka huu mkoani Manyara.
Aidha ametoa rai kwa Wananchi wote kuimarisha usawa na kutokomeza ukatili wa kijinsia na unyanyapaa, kuimarisha lishe
na kuzuia rushwa kwa maendeleo ya Taifa.
Akizungumzia ujumbe mkuu wa Mwenge wa Uhuru mwaka huu,
Waziri Mkuu Majaliwa amesema, unazingatia umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa Taifa.
Ameongeza kuwa ujumbe huo unalenga kuwaelimisha na
kuwahamasisha Wananchi wote kushiriki kikamilifu katika harakati za kutunza vyanzo vya maji.
Baada ya kuwashwa, Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa kwa
vijana sita wakiongozwa na Abdallah Shaibu kutoka mkoa wa
Kaskazini Pemba, ambao watakuwa na jukumu la kuukimbiza
katika mikoa yote nchini.
Viongozi mbalimbali wa mikoa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. @anthony_mtaka wameshiriki ushuhudiaji wa uwashawaji wa Mwenge wa Uhuru 2023.
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa inatarajia kupokea Mwenge wa Uhuru Aprili 25, 2023 ukitokea Mkoa wa Ruvuma.
@ortamisemi @gersonmsigwa @maelezonews @chrispin_b__kalinga @makambakotc
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.