Wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya Ludewa leo Novemba 26, 2022 wameshiriki katika zoezi la kufanya usafi wa mazingira kutoka kwenye maeneo yao yanayowazunguka.
Zoezi hilo limefanyika kuanzia saa moja kamili asubuhi hadi saa nne kamili asubuhi ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kila mmoja kushiriki kufanya usafi kila jumamosi ya kila mwisho wa mwezi.
Afisa Usafi na Udhibiti Taka wa Wilaya ya Ludewa Bw. Kibasa amesema kuwa, mbali ya kwamba kufanya usafi kunafanya mazingira yapendeze na pia kuondao magonjwa yanayosababishwa na kuzungukwa na mazingira machafu, lakini pia zoezi la kufanya usafi kwa pamoja linajenga umoja na mshikamono na kuondoa matabaka katika Jamii yetu.
Kibasa amewasihi wananchi kufanya usafi wa mazingira na kuyapenda mazingira yao siku zote na kujitokeza kufanya usafi kila inapofika jumamosi ya mwisho wa mwezi bila kutegemea, wala kujali uwezo wa mtu, hadhi ya Mtu, cheo au nafasi ya mtu katika jamii.
Mtaa wa Mkondachi Wilayani hapo ni mtaa uliowahamasisha wananchi wao kufanya usafi si wakubwa wala watoto wote wameshiriki kuyaweka mazingira kuwa safi na mtaa wa Kilima hewa kuzifanya barabara na sehemu za biashara kuwa safi muda wote.
Mwalimu wa shule ya sekondari ya Ludewa Sekondari Bi. Clara Mbwaga amesema ufanyaji usafi wa kila mwisho wa mwezi kwenye mtaa wa Mkondachi ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya viongozi na pia ni wajibu wao kama mtaa kuufanya mtaa huo kuwa safi muda wote kwani kwa kufanya hivyo kunaufanya mtaa huo wote na viunga vyake kuwa safi.
"Binafsi mtaa wetu wa Mkondachi ni mtaa unaojitahidi kuwa safi muda wote kwasababu eneo hili kila mwananchi anatambua umuhimu wa usafi, mfano ninapo ishi mimi kila mmoja anatambua umuhimu wa usafi na si kusubiri mwisho wa mwezi, tumepana elimu ya usafi wa mazingira na wote tumeonesha kujitambua na kuyadhamini mazingira tunayoyaishi, amesema Mwalimu Clara
Kwa upande wake Mtumishi mmjoawa Afya kutoka katika hospitalia ya Wilaya ya Ludewa anayeishi mtaa wa Mkondachi Bi. Joyce amejumuika na familia yote inayoishi katika nyumba ya moja ya kunga wamejihamasisha kufanya usafi wa mazingira na kuchoma takataka kavu na karatasi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukipokea kifuku (msimu wa mvua
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.