Na. Chrispin Kalinga
Ikulu mpya ya Chamwino, Dodoma sasa imezinduliwa rasmi leo Mei 20, 2023 kama ofisi na makazi rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Shughuli ya uzinduzi huo ilianza alfajiri kwa wageni mbalimbali kuanza kuwasili katika viwanja vya Ikulu mpya huku wageni mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwasili saa 4:15 asubuhi na kupokelewa na makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wastaafu akiwemo Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Mhe. Jakaya Kikwete.
Mara Baada ya kupokelewa, Mheshimiwa Rais Samia alikwenda katika jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya kupokea heshima ya kijeshi. Baada ya heshima hiyo, Mheshimiwa Rais Samia alikagua gwaride lililoandaliwa maalumu kwa shughuli hiyo.
Aidha Mheshimiwa Rais Samia alikwenda kupanda mti wa kumbukumbu ulio mbele ya jengo la Ikulu ya Chamwino ambalo lilianza kujengwa mwaka 2020 na kukamilika miezi 30 baadaye.
Baada ya hatua hiyo, Rais Samia na viongozi wengine walisimama mbele ya jengo la Ikulu kushuhudia bendera zikipandishwa juu ya mnara wa jengo hilo huku baragumu likipigwa. Bendera tatu zilipandishwa ambazo ni bendera ya Rais, bendera ya Taifa na bendera ya Afrika Mashariki.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.