Na. Chrispin Kalinga
Afisa Mtenda wa Kata ya Ludewa Ndg. Alanus Mbunda wakati akihojiwa na waandishi wa Habari katika ziara ya Afisa Habari na Mawasiliano Serikalini iliyoanza tarehe 01 Septemba 2023 ya kutembelea miradi inayotekekelezwa kwenye Tarafa ya Mawengi na ziara hiyo iliyomilika tarehe 04 Septemba 2023 alisema kuwa, serikali ya awamu ya sita ndani ya kata ya Ludewa imeleta fedha za kuteketeza Miradi mbalimbali zaidi ya shilingi Bilioni 10 katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutekeleza miradi ya Miundombinu ya Barabara, Elimu, Afya, Maji pamoja na Mawasiliano.
Wakati wa kujibu swali aliloulizwa na waandishi wa Habari lililohoji kuwa, kwa kipindi cha miaka miwili ya Rais Samia Nini kimefanyika kwenye kata yako? Mtendaji Mbunda alisema kuwa, "Zaidi ya Bilioni 10 zimeletwa kwenye kata ya Ludewa, na ninaimani kuwa kata ya Ludewa ni miongoni mwa Kata zilizopokea fedha nyingi kiliko zote kwenye kata za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, hapa Ludewa tumepewa fedha ya ujenzi wa kipande cha lami cha kwenda Manda, kipande cha lami cha kwenda Lupingu na bado Barabara za mitaa ukianzia hapa Mkondachi imewekwa lami,ukienda kwenye Miundombinu ya Maji hapo tumepewa zaidi ya Bilioni 5 za Mradi wa Maji pale kilimahewa, tumejengewa Mnara wa simu kule Kijiji cha Ludewa K, bado serikali imetujengea Ikulu ndogo hapa Mjini, Jengo la utawala la Ofisi za Mkurugenzi linabadilisha taswila ya mji kwa kupendeza kwake hivyo ninakila sababu ya kupiga kigeregere kwenye miradi hii mikubwa, yote hii ni kwa jitihada za viongozi mahiri, wachapakazi na wenye kupenda Maendeleo wakiongozwa na Amiri Jeshi Mkuu, Rais wetu mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan". alisema Mbunda
Aliendelea kwa kusema kuwa "Ukija kwenye Jimbo yupo Mbunge Mhe. Joseph Kamonga kazi yake inaonekana na sisi wanaludewa tunamshukuru sana kwasabu bila ya yeye kupaza sauti haya mafanikio tungeyasikia kwa mbali, lakini kwasababu yupo anachapa kazi kwa kushirikiana na waheshimiwa Madiwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Wise Mgina kazi inaendelea kwa Kasi" alimesema Bw. Mbunda
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.