Mazingira ni ghala la kuhifadhi malighafi zote zinazohitajika kuendeleza uhai wa viumbe hai na mfumo-ikolojia.
Mahitaji yote ya binadamu hutunzwa ndani ya mazingira. Mazingira yanahusisha maumbile halisi yawazungukayo binadamu ikiwa ni pamoja na hewa, ardhi, maji, tabianchi, sauti, mwanga, harufu, ladha, vijiumbe, hali za kibiolojia za wanyama na mimea, rasilimali za kitamaduni na masuala ya uchumi jamii na inahusisha mazingira asilia na yaliyoundwa na binadamu na jinsi yanavyoingiliana.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mhe. Wise Mgina ameshiri kikao cha wataalamu waliokuja kutoa elimu ya Maji na Usafi wa Mazingira kilichofanyika leo Julai 6, 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kikiongozwa na Mhadhiri DR. Francis Moyo kutoka katika chuo cha chuo cha Nelson Mandela African Institution of Science and Technology
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.