Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Victoria Mwanziva awaomba Wataalamu wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kushirikiana na Waheshimiwa Madiwani katika utekelezaji wa majukumu yao.
Ameyasema hayo leo Mei 13, 2023 katika Mkutano wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani wa Robo ya tatu ya mwaka 2022/2023 wa Kipindi cha Kuanzia Januari hadi Marchi, 2023 wa Tarehe 13 Mei, 2023 Uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Mhe. Victoria Mwanziva amesema kuwa, Madiwani ndio wenye wajibu wa kuzisemea taarifa za utekelezaji kwa Wananchi hivyo ni haki yao kupewa taarifa zote za maeneo yao kwa wakati.
“Tuongeze ushirikishwaji wa taarifa kwa Waheshimiwa Madiwani lengo ni kuwa na uelewa wa pamoja wa miradi ya maendeleo, kwasababu Madiwani ndio watakao zisemea hizi taarifa kwa wananchi.” Amesema Mhe. Mwanziva
Aidha amewataka Wataalamu kutoa taarifa kwa madiwani wa maeneoe husika kila wanapo kwenda kufanya shughuli za maendeleo kwenye kata husika.
“Ni marufuku kwa mtaalamu kwenda eneo fulani bila kutoa taarifa kwa Diwani wa eneo husika ili mfanye kazi vizuri” amesema Mheshimiwa Victoria Mwanziva.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.