Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Andrea Tsere leo Mei 03, 2022 ameongozana na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo wakiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mhe. Wise Mgina, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndugu Sunday Deogratias, Afisa Ardhi na Maliasili Bw. Girbeth Ngailo na wengineo, ziara hiyo imefanyika katika Kata ya Mundundi kwalengo la uhamasishaji wa uwekaji wa namba katika nyumba za wananchi na uwekaji vibao vinavyo tambulisha barabara.
Wakati akihutubia wannchi Mhe. Andrea Tsere amewasihi wananchi kujiandaa na zoezi la Sensa ambalo linatarajia kufanyika rasmi mwezi wa nane na akaongeza kwa kusema kuwa licha mambo mengine yote yanayo endelea amewataka wazazi na walezi kuwapa watoto chakula kwa wakati ili kuondokana na lishe duni huku akiongeza kwa kusema kuwa,Wilaya ya Ludewa ina kila aina ya chakula na inakila sababu ya kutokomeza Udumavu kwa kushirikiana na wazazi na wataalamu wataendelea kutoa elimu ili kuutokomeza Udumavu ndani ya Wilaya ya Ludewa
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya akaongeza kwa kusema kuwa wananchi wote wa Wilaya ya Ludewa wanapaswa kuendelea kujilinda na magonjwa ambukizi kama vile UVIKO 19 kwa kuwahamasisha wananchi wote kuchanja kwasababu chanjo hiyo haina madhara yoyote.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.