Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Andrea Tsere leo Juni 13, 2022 ameaomba wananchi wote wa Wilaya ya Ludewa kujitokeza siku ya kesho kuchangia damu.
Ameongea kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa Habari Ofisi kweke kwa kusema kuwa kesho Juni 14, 2022 ndio siku ya kilele cha kuchangia damu salama Duniani, hivyo niwaombe wananchi wote mjitokeze kuchangia damu katika vituo vya Afya vyote vilivyopo kwenye maeneo mbalimbali ya Wilaya yetu.
Sambamba na hayo Mhe. Andrea Tsere amesema kuwa Licha ya siku hii Duniani ambapo kilele chake inafanyikia Songwe niwaombe wananchi wote tuendelee kuchangia damu kwa hiyari yetu kwani kwa kufanya hivyo inasaidia kuwasaidia watu wenye uhitaji wa Damu na tukawa tumeokoa maisha yatu.
Hali kadhalika akatumia nafasi hiyo kuwakumbusha wnaanchi wote wa Wilaya ya Ludewa Kujiandaa na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 na amewaomba wananchi wote siku hiyo ukifika kila mwananchi ahakikishe anahesabiwa yeye na familia yake.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.