Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere akiwakilishwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa Bw. Linus Malamba ameongoza kikao kazi cha wadau wa Kilimo kinacho endeshwa na Shirika la Care myAgro.
Kikao hicho wameshiriki wajumbe mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Madiwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mhe. Wise Mgina, Watendaji wa Kata pamoja na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kikiwa ni sehemu ya muendelezo wa utekelezaji wa mradi wa Kilimo inayotekelezwa kwenye Tarafa ya Liganga na Tarafa ya Masasi.
Leo oktoba 18, 2022 wasimamizi wa mradi huo kwa ngazi ya Wilaya wametoa mrejesho wa mradi kutoka kata za Manda, Ruhuhu, Masasi, Luilo, Nkomang'ombe, Mundindi na Mavanga.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.