Na Chrispin Kalinga
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mheshimiwa Victoria Mwanziva amewataka wazazi na walezi wa Wilaya ya Ludewa kuchukue hatua stahiki kutatua tatizo la udumavu na kuhimiza lishe bora.
Mikoa yenye kiwango kikubwa cha udumavu zaidi ya wastani wa kitaifa ni pamoja na Mkoa wa Njombe wenye asilimia 50.4
Ametoa wito huo leo asubuhi (Jumatano, Julai 19, 2023) wakati akizungumza na wakazi na Walezi wa Kata ya Ludewa waliofika kupata mafunzo mbalimbali ya lishe yaliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Ludewa yakiongozwa na Wataalamu na wasimamizi wa Lishe wa Wilaya ya Ludewa.
“Taarifa zilizopo zinaonesha hali ya lishe miongoni mwa Watoto hairidhishi kutokana na kuathiriwa na tatizo la udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, uzito pungufu na ukondefu sasa tunapaswa kuchukua hatua stahiki kusimamia suala zima la watoto lakini pia Lishe bora kwa mama mjamzito’ amesema Mhe. Victoria Mwanziva.
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Wilaya Mhe. Victoria amesema “Wananchi wenzangu, sasa ni wakati muafaka wa kubadili mitindo ya maisha yetu kuanza kula mlo kamili sambamba na kuepuka vyakula vyenye mafuta mengi, sukari nyingi, pombe na sigara,” amesisitiza.
Kwa Upande wake, Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Mhe. Joseph Kamonga amesema dhamira ya Serikali ya awamu ya sita ni kuboresha huduma za kijamii na maisha ya Watanzania katika sekta za elimu, afya, maji na barabara. Hatua hizo, zinakwenda sambamba na uwekezaji mkubwa katika usafiri na usafirishaji nishati ya umeme, na akaongeza kuwa, kunahaja sasa ya wazazi na walezi kuzingatia mlo kwa watoto na wajawazito ili kuleta kizazi chenye afya bora.
Elimu ya lishe imeendelea kutolewa vijiji vyote 77 vya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na wazazi kuhimizwa kuzingatia mlo bora kwa motto ili kuondokana na udumavu, Mkutano huo umeudhuriwa na viongozi wa chama cha mapinduzi akiwepo Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Ndg. Gervas Ndaki, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Sunday Deogratias, viongozi wa Kata ya Ludewa akiwemo Diwani wa Kata hiyo.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.