Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka leo tarehe 17/08/2022 amefanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Jabir Mwadini ambaye amefika na mwekezaji anayehitaji kujenga kiwanda kitakachoongeza thamani ya zao la Parachichi mkoani Njombe.
Kwa pamoja wametembelea moja ya kiwanda kilichopo Mkoa wa Njombe kinachojulikana kwajina la AvoAfrica.
Sambamba na hayo wamemtembelea mkulima anayefanya vizuri kwenye kilimo cha Parachichi Mzee Msuya akiwa na zaidi ya Hekari 50, na kuona fursa kubwa ya usafirishaji wa parachichi kama tunda,na uchakataji wa parachichi katika kutoa bidhaa kama mafuta, juices,na vipodozi.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Mtaka amesema kuwa "Nitumie nafasi hii kuendelea kuwakaribisha watanzania na sekta binafsi kwenye uwekezaji wa zao hili,ama kwa kulilima au kwa kuliongezea thamani"
Akaongeza kwakusema kuwa, "Baada ya Saudia ambako Parachichi za Njombe zina soko kubwa sana,tunajipanga kufungua masoko mengi zaidi bara la Ulaya, ASIA na America.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.