Serikali ya mkoa wa Njombe imezindua zoezi la utoaji wa chanjo ya ugonjwa wa polio awamu ya pili kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano zoezi ambalo litafanyika kwa siku nne.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba ameongoza zoezi hilo kwa kutoa chanjo kwa watoto kwa ushirikiano na wataalamu wa afya katika kituo cha afya cha Njombe mjini na kubainisha kuwa katika awamu ya pili tena watoto zaidi ya laki moja na kumi wanatarajia kupata chanjo hiyo.
“Ni muhimu kulinda na kukinga watoto wetu kwa kuwa hii ndio Tanzania ijayo,tunatakiwa kuwalinda watoto wetu”alisema Kindamba
Vile vile Waziri Kindamba amewapongeza na kutoa zawadi kwa wanaume waliojitokeza kufikisha watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kupata chanjo ya ugonjwa wa Polio kwa njia ya matone.
“Wababa kama hawa wamebaki wachache sana,baba ambaye anamsindikiza mama ili mtoto apate chanjo,sina shaka baba wa namna hii hata mama alipokuwa mjamzito alikuwa anaambatana naye kwenda Kliniki”alisema Kindamba
Kindamba amesema katika awamu ya kwanza mkoa wa Njombe umevuka lengo kwa kuchanja watoto kwa 116% huku akibainisha kuwa zoezi hilo linaendelea kwa mikoa minne ya Njombe,Mbeya,Ruvuma na Songwe ambayo ipo jirani zaidi na nchi ya Malawi ulikoanza kuibuka ugonjwa huo.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.