Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndugu Sunday Deogratias leo Agasti 02, 2022 amewakaribisha Watanzania kuwekeza wilayani Ludewa.
Hayo ameyasema alipokuwa kwenye viwanja vya maonesho ya nanenane Jijini Mbeya kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa wakati wakitembelea na kuyaona mazao mbalimbali yanayolimwa Wilayani Ludewa.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa amewawaeleza Wananchi waliotembelea banda hilo kuwa, Wilaya ya Ludewa ni miongoni mwa Wilaya zinazolima mazao tofauti tofauti hapa nchini Tanzania yakiwemo, Mahindi, Maharage, Korosho,Kahawa,Alizezeti,Mpunga,Ngano na mengineyo.
Sambamba na hayo akaongeza kwakusema kuwa, *Wilaya ya Ludewa inamaeneo mengi ya Kilimo hivyo nitumie nafasi hii kuwakaribisha Wilayani Ludewa kuja kuwekeza katika sekta ya Kilimo na sisi Kama serikali tupo tayari kutoa ushirikiano kwayeyote anaehitaji kuja kuwekeza.*
Mwisho akamaliza kwakusema kuwa *licha ya uwekezaji mkubwa wa kilimo tunawakalibisha kuja kuwekeza Ludewa katika sekta ya Utalii, Wilaya ya Ludewa tupo na madini mengi yakiwemo Chuma kutoka Liganga na Makaa ya mawe kutoka mchuchuma
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.