Novemba 09,2022 Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Mhe. Pindi Chana alifungua rasmi maonesho ya vivutio vya Utalii nyanda za juu Kusini yanayotambulika kwa Utalii Karibu Kusini katika viwanja vya maonesho Mkoani Iringa.
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imeshiriki Uzinduzi wa Maonyesho hayo yanayofanyika kwa siku tano kuanzia tarehe 09/11/2022 hadi tarehe 13/11/2022.
Wakati akifungua maonesho hayo Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dk. Pindi Chana alieleza kuwa uwepo wa vivutio vizuri na vya kipekee vya Utalii katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania ambayo ni Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Mtwara,Lindi, Morogoro, Songwe, Rukwa na Katavi ni fursa kwa wananchi wa mikoa hiyo kuendelea kunufaika kiuchumi kutokana na shughuli za utalii zinazofanyika.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndugu Sunday Deogratias ambaye ameambatana na Wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa wakiwa wamebeba vitu mbalimbali kwaajili ya maonesho katika viwanja hivyo wakati akifanya mahojiano na vyombo vya habari hapo jana alisema kuwa, Ushiriki wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwenye maonyesho hayo ni kutoa elimu lakini pia kubaini changamoto mbalimbali hususani katika sekta ya Utalii ili kuzifanyia kazi na kuhakikisha watalii na jamii nzima inayozunguka inatembelea vivutio vya utalii ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Aidha akaongeza kwakusema kuwa uwepo wa wataalamu kwenye maonesho hayo kutaleta tija kwa Halmashauri kwani wanapata fursa ya kuwatangazia Watanzania na kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa haswa katika sekta ya Utalii ikiwa ni pamoja na Ziwa Nyasa lakini pia kunawapa fursa Watanzania kutembelea Wilaya ya Ludewa ili kufanya Uwekezaji katika sekta ya Kilimo na Uwekezaji katika sekta ya Madini.
Sambamba na hayo Mkurugenzi huyo akatumia nafasi hiyo kuwaeleza Watanzania kuwa Wilaya ya Ludewa inauhakika wa maeneo ya uwekezaji na serikali ipo tayari kuwapa ushirikiano Wawekezaji wote watakao kuja kuwekeza ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa haswa kwenye Uwekezaji wa Kilimo, Uwekezaji wa Uvuvi na Mifugo, Uwekezaji wa Kilimo cha Mita na Uwekezaji katika sekta ya Madini.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.