Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratias ametoa
onyo kwa kiongozi yeyote ngazi ya kata na kijiji
ambaye atabainika kuwafumbia macho watu
wanaoharibu rasilimali za maji kwa kuchoma
moto na kuwataka wachukuliwe hatua kali
kisheria kwa kuwafikisha mahakamani.
Hayo ameyasema katika uzinduzi wa mafunzo
ya watumia maji bonde la Ziwa Nyasa ambayo
yamehusisha viongozi mbalimbali, wataalam
pamoja na wadau katika kuandaa mpango
shirikishi wa vyanzo vya maji, katiba na uundaji
wa jumuiya ya watumia maji bonde dogo la mto
Mchuchuma.
Aidha Sunday ameongeza kuwa kuna kamati za
uchomaji moto ambazo zimeundwa kwa kila
kijiji kwa lengo la kusimamia shughuli hizo
za uvhomaji moto ambapo kwa mtu yeyote
anayehitaji kusafisha eneo lake ikiwemo
mashamba wanapaswa kupata kibali na
kusaidiwa na jumuiya hizo ili kukamilisha
shughuli zao pasipo uharibifu wowote.
"Watu wanao bainika kufanya uharibifu
wamekuwa wakilipiswa faini ya sh. 300,000
lakini imeonekana watu hao hawakithamini kiasi
hicho cha fedha na ndiomaana matukio haya
yameendelea kutokea hivyo kwa sasa watu hawa
wanapaswa kufikisha mahakamani ikiwezekana
wahukumiwe kifungo"
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.