Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg.Sunday Deogratias leo Novemba 25 ameshiriki kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Njombe (RCC).
Pamoja na mambo mengine zimewasirishwa taarifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na taarifa ya elimu ambapo Afisa elimu mkoa wa Njombe Nelasi Mulungu amesema kuwa
Jumla ya wanafunzi 963 wa shule za sekondari mkoa wa Njombe kati yao wavulana 584 na wasichana 379 sawa na asilimia sita hawakufanya mitihani yao ya kidato cha pili kutokana na sababu mbalimbali.
Akizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri mkoa RCC, Afisa elimu mkoa wa Njombe Nelasi Mulungu alisema wanafunzi hao walianza kidato cha kwanza vizuri lakini walivyoingia kidato cha pili wakawa wamepotea.
"Wanafunzi waliofanya mtihani 2022 waliandikishwa shule ya sekondari mwaka 2021,kidato cha kwanza wakiwa jumla ya wanafunzi 15,256 kati yao wavulana 6,664 na wasichana 8,546 hivyo walistahili kufanya mtihani wa kidato cha pili mwaka 2022"alisema Mulungu.
Mulungu alisema watoto wengi watoro ni wavulana ambao inadaiwa kuwa wanakwenda kufanya vibarua mikoa ya jirani.
"Tumewajulisha mamlaka za halmashauri na wakuu wa wilaya kuwatafuta ili kurudi shule, kwa sababu mh Rais ametoa ridhaa kwa watoto wote ambao wameacha shule kwa sababu mbalimbali warudi shuleni,awe wa sekondari awe wa shule za msingi kwa hiyo mamlaka husika zinaendelea kuwatafuta"alisema Mulungu.
Ofisa ustawi wa jamii mkoa wa Njombe Subilaga Mwaigwisya,alisema changamoto kubwa inasababishwa na wazazi kuwaachia majukumu ya familia watoto wa kiume.
"Tumekua na ugomvi mkubwa na familia wazazi hasa kwa watoto wa kiume,baada ya baba labda kuondoka alafu yule mtoto wa kiume anachukua majukumu kama baba au wakati mwingine anaenda kufanya shughuli za kiuchumi zinaweza zikawa ni zake au za familia nzima kwa hiyo wengi wao wanaenda kujihusisha na shughuli za kiuchumi,kwenye kubeba mbao,biashara ndogondogo"alisema Mwaigwisya.
Hata hivyo alisema"Lakini kwa watoto wa kike ukiangalia hiyo takwimu tunao watoro lakini tunashindwa kujua wapo wapi kwa sababu hatuna ndoa za utotoni wala watoto wa kike wanaofanyishwa kazi kwa sababu tunafanya ukaguzi hata nyumba kwa nyuma ili mtoto wa kike aweze kupata elimu"alisema.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.