• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Ludewa District Council
Ludewa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uchumi
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
      • Maji
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafi na Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Shughuli za Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Samaki
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Huduma za UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
      • Kazi za Mwenyekiti Ofisini
  • Miradi
    • Miradi Iliyo Kwenye Mpango
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Habari Picha

MKOA WA NJOMBE UNAONGOZA KWA IDADI KUBWA YA MADINI MKAKATI NCHINI.

tarehe Iliyowekwa: September 26th, 2023

Njombe Tanzania

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka amepokea Kitabu cha madini yapatikanayo Tanzania

Utafiti wa awali uliofanywa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ulibaini kuwa Mkoa wa Njombe unaongoza kuwa na idadi kubwa ya Madini Mkakati kati ya Mikoa yote nchini.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Sehemu ya Jiolojia kutoka GST Maswi Solomon baada ya kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka kwa lengo la kuwasilisha Vitabu vinavyoonesha Madini yapatikanayo Tanzania.

Mtaka amesema, Mkoa wa Njombe una jumla ya Wilaya nne ambazo ni Njombe, Makete, Ludewa na Wanging'ombe ambapo Kitabu hicho kitawasaidia wananchi wa Mkoa huo na Wilaya zake kuvutia Wawekezaji Mkoani humo.

Aidha, ametoa wito kwa GST kutumia uzoefu walionao kwenye madini yaliyozoeleka nchini na kuupeleka kwenye Madini Mkakati ili kuepuka changamoto na migogoro iliyotokea huko nyuma hususan kwenye madini ya dhahabu.

Pia, Mtaka ameipongeza GST kwa kuchora Ramani za Madini nchi nzima na kuishauri taasisi hiyo kuendelea kufanya tafiti za madini, maji na nishati katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wake, Meneja wa Sehemu ya Jiolojia kutoka GST Maswi Solomon amesema kufuatia uwepo wa Madini mengi ya kimkakati katika Mkoa  wa Njombe Kitabu hicho kitasaidia kutambua aina ya madini yaliyopo na kusaidia kuvutia Wawekezaji Mkoani humo ili kufanya utafiti wa kina kwa kuwa utafiti wa kina na uvunaji wa madini mkakati huhitaji teknolojia ya juu ambayo wachimbaji wadogo wanashindwa kumudu gharama zake.

Pamoja na Mambo mengine, Maswi ametaja baadhi ya Madini Mkakati yaliyopo Mkoani humo ambapo ni pamoja na chuma, makaa ya mawe, titanium, vanadium, chromium, PGM, REE, shaba, Manganese, gesi ya methane na dhahabu.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI January 10, 2025
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI III, NA WITO WA USAILI WA ANA KWA ANA KWA WALIOCHAGULIWA November 11, 2021
  • TAADHARI YA UGONJWA WA POLIO LUDEWA March 24, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA KATIBU MAHSUSI III NA DEREVA II May 25, 2022
  • Tazama zote

Habari za Punde

  • MKUU WA WILAYA LUDEWA AUNGANA NA WANANCHI KUADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUSAFISHA MAZINGIRA

    June 05, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA WILAYANI LUDEWA NA KUTEMBELEA MIRADI MITANO(5)

    May 07, 2025
  • WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA MH. SELEMANI JAFO AAHIDI KUANZISHWA KWA MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA HIVI KARIBUNI

    February 19, 2025
  • ZIARA YA WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA, MHE. DKT. SELEMANI JAFO MKOANI NJOMBE, WILAYANI LUDEWA.

    February 17, 2025
  • Tazama zote

Video

Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Dira na Dhima
  • Utawala na Rasilimali Watu
  • Historia
  • Misingi Mikuu
  • Orodha ya Madiwani
  • Miradi Iliyokamilika

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais IKULU
  • Tovuti Kuu ya Wananchi
  • Wizara ya Afya
  • Tume ya Taifa ya Uchaguzi
  • TANePS

Wanaotembelea Tovuti

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ludewa - Njombe

    Sanduku la Barua: 19

    Simu: 026-2790120

    Simu ya Rununu:

    Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.