Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa kiongozi wa Tanzania na aliiongoza Tanzania, na kabla ya hapo Tanganyika, kuanzia 1960 hadi alipostafu mwaka 1985.
Anatambuliwa kuwa ndiye Baba wa Taifa, Baba yake alikuwa Nyerere Burito (1860 -1942), chifu wa kabila la Wazanaki.
Anafahamika zaidi kwa jina la Mwalimu – taaluma yake ya zamani kabla ya kujiunga na harakati za ukombozi.
Mwalimu Nyerere alipata elimu yake katika chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda na pia katika chuo kikuu cha Edinburg cha Uingereza.
Alisaidia kuunda chama cha Tanganyika African National Union (TANU), na Tanganyika ilipopewa serikali mwaka 1960, Mwalimu Nyerere alikuwa Waziri Kiongozi, na kuiongoza nchi ya Tanzania kwenye uhuru wake mwaka moja baadaye, na kuwa waziri mkuu wa kwanza.
Tanganyika iligeuka na kuwa Jamhuri mwaka 1962 na Mwalimu Nyerere akawa Rais wake wa kwanza.
Mwaka 1964, Tanganyika iliungana kisiasa na Zanzibar na kuzaa Jamhuri ya Tanzania, ambako Nyerere aliendelea kuwa Rais hadi alipon’gantuka mwaka 1985.
Mwalimu Nyerere alifariki dunia Oktoba 14, 1999 akiwa na umri wa miaka 77.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.