Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alieleza kufurahishwa na kukamilika kwa mradi wa maji nchini
Amesema hayo jana Machi 22, 2022 katika maadhimisho ya siku ya Maji Duniani .
Na kwaupende wetu Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ujenzi wa Miundombinu ya maji inaendelea ikiwa ni pamoja na kupatiwa fedha za kukamilisha miradi hiyo, na kwa mwaka 2021 miradi iliyo tekelezwa kwa ukarabati na upanuzi ni, Ujenzi na Ukarabati wa mradi wa maji Kimelembe-Mkomang'ombe ambapo mradi huo umekamilika kwa thamani ya sh.782,846,976.00 na Ujenzi wa mradi wa maji Iwela ukiwa umekamilika kwa thamani ya sh.1,440,000,000.00
Pamoja na hiyo miridi iliyo kamilika ni pamoja na mradi wa maji Mbugani,Ukarabati wa Tank la maji Ludewa Mjini HIMA,Ukarabati wa Mfumo wa maji Mlangali na wakati huo Mradi wa Ujenzi wa mradi wa maji Lupingu ukiwa upo hatua za mwisho kwenye utekelezaji,na ujumla wake kwa miradi tajwa hapo juu itakuwa imegharimu sh.2,919,599,872.00
Na kwa mwaka 2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imepokea fedha ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji kiasi cha sh.2,108,673,191
Ambapo miradi inayo fikiwa nipamoja na Ujenzi na uboreshaji wa mfumo wa Maji Ludewa Mjini,Ujenzi wa mradi wa madope,Ujenzi wa mradi wa maji Madindo,Ujenzi wa mradi wa maji Ibumi,Ujenzi wa mradi wa maji Lifua na Ujenzi wa mradi wa maji Ihela.
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa tunamshukuru Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha ya kutekeleza miradi mikubwa ya maji.
Endelea kutembelea Mitandao yetu ya kijamii kwa habari za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.