Mhe.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Wise Mgina ambaye pia ndiye Diwani Kata ya Mundindi Leo Machi 18, 2022 Wakati wa kukabidhiwa bweni pamoja na Pikipiki Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa amelipongeza Shirika la Padeco kwa mchango wao mkubwa haswa katika kufanikisha ujenzi wa bweni hilo utakao saidia watoto wanao soma katika shule hiyo ya msingi ya watu wenye mahitaji maalum
Lakini pia akaongeza kwa kusema kuwa Shule hii ya watoto wenye ulemavu kwa Wilaya yetu ya Ludewa inapokea watoto kutoka maeneo tofauti nikiwa na maana ya ndani ya halmashauri ya Wilaya yetu na Mkoa mzima wa Njombe na pia saivi shule hii inapokea watoto kutoka nje ya Mkoa wa Njmbe,hivyo PADECO mchango wenu huu ni mkubwa tunawaomba msichoke kuja kuleta msaada na mahitaji mengine kadri mnavyo jaliwa.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa licha ya Shirika la Padeco kujenga bwini hili na serikali yetu pia imejenga jengo lingine kubwa ambalo lipo hatua za mwisho,hivyo nikiwa kama Mwenyekiti wa Halmashauri kwa umuhimu wa Shule hii,serikali inakila sababu ya kuona umuhimu wa kuongeza walimu katika shule hii ili waweze kutosheleza kuwahudumia watoto hawa,sambamba na hayo nitaenda kuishawishi serikali ione umuhimu wa kujenga na sekondari hapa,maana eneo bado lipo kubwa,na linauwezo wa kutosheleza kujenga shule ya sekondari ya watu wenye mahitaji maalumu,hii itasaidia mwenendo mzuri kwa wanafunzi wanao faulu kujinga na kidato cha kwanza,na sio hivyo tu bali nitaishawishi serikali kujenga chuo cha ufundi cha watu wenye mahitaji maalum ili waweze kujifunza mambo mbalimbali.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.