Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka alizitaka halmashauri mbalimbali za mkoa huo, kukuza uchumi wao kwa kutumia rasilimali zilizopo katika halmashauri husika.
Mtaka aliyasema hayo baada ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Waziri Waziri Kindamba ambaye anaenda kuwa mkuu wa mkoa wa Songwe ambao ulihusisha viobgozi mbalimbali ngazi ya wilaya na mikoa zikiwemo taasisi binafsi.
Mtaka alisema viongozi pamoja na wananchi wanapaswa kuwa wabunifu katika kuanzisha vyanzo vya mapato kulingana na ardhi pamoja na hali ya hewa iliyopo kwakuwa ina uwezo wa kuhimili mimea pamoja na mifugo.
” Halmashauri zilizo nyingi zimeishia kuwa na mradi wa choo, Halmashauri zinapaswa kujisimamia katika miradi ya maendeleo kutoka katika mapato ya ndani na ili kuweza kuwa na mapato ya kutosha hakikisheni mnatambua fursazilizopo katika halmashauri zenu na mhamasishe watu wawekeze katika fursa hizo”. Alisema Mtaka.
Aliongeza kuwa hali ya hewa ya Njombe na ardhi ni mtaji tosha wa kuwafanya wananjombe wanakuwa kiuchumi hivyo hawezi kukubali kuona wananchi wa mkoa huo wanaishi kinyonge na kuendelea kutengeneza wazee watakaokuwa wanudaika wa TASAF katika siku za usoni.
Aidha katika makabidhiano hayo ya ofisi aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Waziri Kindamba alimuomba Kindamba kuendeleza mipango ya naendeleo pale alipoishia ili kuiletea maendeleo Njombe hasa katika ujenzi wa kiwanja cha ndege na kufuatilia wawekezaji waliojitokeza katika sekta ya kilimo cha mazao mbalimbali ikiwemo parachichi, Soya pamoja na ngano.
Kindamba alisema kuwa Njombe kuna uwanja wa ndege ambao hutumika isivyo sahihi ambapo wananchi hutumia kwa kukatiza kama njia huku katika sekta ya kilimo tayari kuna wawekezaji ambao wamekuja kuona maeneo na kuahidi kurudi kuwekeza.
“Ukiangalia uwanja wetu wa ndege unatumika kama njia ya watembea kwa miguu, bajaji, pikipiki na wengine hutumia kuanika nguo kitu ambacho kilinifanya niweke uzio na kuweka ulinzi watu wasiendelee na natumizi hayo na kwa atakayebainika anapigwa faini”, Alisema Kindamba
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.