RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN WAKATI AMEZINDUA SOKO KUU LA NJOMBE NA KUYASEMA HAYA
1. Kurasimisha sekta isiyo rasmi ndio adhma ya Serikali, wafanyabiashara wanaofanya biashara katika soko kuu la Njombe hawakuwa rasmi lakini kwa sababu wamejengewa soko, wamewekwa sehemu moja na wamewekewa huduma zote wameshakuwa rasmi.
2. Adhma ya Serikali ni kuwaweka Wafanyabiashara pazuri, tunataka kutoka kwenye jina la Wamachinga mpaka kuwa wafanyabiashara rasmi.
3. Nataka viongozi wa Mkoa kuangalia nafasi katika soko hili ili itengwe sehemu kwa ajili ya kuwaweka watoto wa wafanyabiashara mahali pamoja na kupewa huduma stahiki huku biashara zikiendelea.
4. Kutokana na huduma hiyo, Wafanyabiashara watatakiwa kuchangia kidogo kwa ajili ya matunzo ya watoto.
5. Serikali itaendelea kujenga masoko ya aina hii katika miji mbalimbali ili wafanyabiashara na wananchi wa Tanzania wapate huduma mahali pazuri.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.