Na Chrispin Kalinga
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amezisisitiza Wizara kusimamia sheria na kutekeleza miradi iliyopo kwenye bajeti ya mwaka mpya wa fedha 2023/2024, na kuhakikisha fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara ya Makambako hadi Songea zinapatikana na matengenezo yanafanyika.
Mhe. Dkt. Mpango amesisitiza hayo leo aliposimama kuwasalimia wananchi wa Mkoa wa Njombe,eneo la tanki la maji katika Halmashauri ya Mji Makambako akielekea Songea mkoani Ruvuma.
Amesema kuwa,ipo haja kwa Wizara ya kilimo kusimamia sheria ili kutokomeza rumbesa,uuzaji wa mazao shambani na walanguzi wa mbolea ili mkulima anufaike kupitia kilimo na kufaidi jasho lake,kwa kuhakikisha mazao yote ikiwa ni pamoja na viazi vinapimwa kwa vipimo sahihi,walanguzi wa mbolea wanakoma kwa kuwachukulia hatua za kisheria bila kuwachekea.
Pia,amewataka wakulima wa zao la parachichi Mkoa wa Njombe kutouza parachichi ambazo hazijakomaa,kwa kushawishiwa na wanunuzi wenye nia ovu ili kuharibu sifa za bidhaa zinazozalishwa nchini ,na kuitaka Wizara ya kilimo kuendelea kutoa elimu kwa wakulima wa zao hilo juu ya athari za uuzaji wa parachichi ambazo hazijakomaa.
Aidha,ameitaka Wizara ya fedha ,kutafuta fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara ya Makambako hadi Songea,kwani barabara hiyo ni kubwa na inatumika kusafirisha mazao ya chakula na bidhaa nyingi kwa ajili ya Uchumi wa Mikoa hiyo na taifa kwa ujumla.
Lakini pia,ametoa wito kwa kina mama kuacha urembo wakunyonyesha kwa kuhakikisha wanakula vyakula vyenye virutubisho kipindi chote cha ujauzito hadi kujifungua,na kunyonyesha watoto kwa muda wa miaka miwili na kuhakikisha watoto wanakula vyakula vyenye virutubisho muhimu kwa afya zao, ili wapate lishe bora na kuwa na afya bora katika ukuaji wao.
Aidha,ametoa rai kwa wazazi kuwasomesha watoto wao kwani ni uwekezaji wa uhakika ,kwa manufaa yao na watoto wao,pamoja na kuchukua tahadhali juu ya maambukizi ya UKIMWI ili kudhibiti maambukizi mapya.
Viongozi mbalimbali kutoka Mkoa wa Njombe wakiwemo viongozi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa wameshiriki mkutano wa Mhe. Dkt. Mpango
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.