Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amesema kilio chake kikubwa katika Jimbo lake Ni changamoto ya miundombinu ya barabara ambayo imekuwa ikikwamisha shughuli za kujitafutia kipato kwa wananchi.
Mbunge Kamonga ametoa kauli hiyo kwenye kikao Cha ushauri mkoa wa Njombe RCC ambapo amesema licha ya serikali kufanyakazi kubwa ya kuboresha miundombinu mbalimbali lakini barabara zimekuwa kilio kikubwa katika Jimbo hilo hasa katika kusafirisha mazao wanayolima kuyapeleka sokoni.
Aidha pia Mbunge huyo amesema katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali wananchi wake wamekuwa wakijitoa kujenga lakini serikali inachelewa sana kupelekea fedha za ukamilishaji wa majengo hayo.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.