Jana Agasti 17, 2022 Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Joseph Kamonga alifanya mikutano miwili ndani ya kata ya Ludewa mjini, Mkutano wa kwanza ulifanyika Mdonga na wa pili ulifanyika sokoni Ludewa mjini
Wananchi wa kata ya Ludewa mjini walimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa jitihada anazoendelea kuzionesha za kutuletea Maendeleo wana Ludewa.
Ziara ya Mbunge ilijikita kwenye ajenda kuu tatu, ya kwanza kuhamasisha shughuri za Maendeleo, kutoa mrejesho wa nini kimefanyika katika vikao vya Bunge, kuhamasisha sensa ya watu na Makazi yaa mwaka 2022.
1.Katika kuhamasisha shughuli za Maendeleo, Mheshimiwa Mbunge alitoa mchango wa Milioni mbili kwaajili ya kuandaa tofali za Ujenzi wa shule.
Milioni 1 uandaaji wa tofali za Ujenzi wa shule ya Msingi Mdonga na milioni 1 kwaajili ya kuandalia tofali za Ujenzi wa shule ya sekondari Ludewa kijijini.
Mheshimiwa Mbunge aliwaomba wananchi kushiriki kikakamilifu katika jambo hili kwani maeneo yote mawili watoto wanasafiri umbali mrefu kwenda kufuata elimu.
2. Mhe. Mbunge alitoa taarifa ya hali ya miradi inayoendelea kutekelezwa na inayo tarajia kuanza kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023
3. Mhe. Mbunge alitowa elimu ya sensa kwa wakazi wa Ludewa na kueleza umuhimu wake katika utoaji wa huduma za kijamii,Hivyo Mhe. Mbunge aliwaomba Wanaludewa kujiandaa kikamilifu kuhesabiwa na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maafisa wa sensa watakao pita kwenye kaya zao siku ya zoezi hilo.
Sambamba na hayo Mhe. Mbunge alitoa mrejesho wa nini amefanya alipokuwa Bungeni na matokea yake yapoje mpaka Sasa
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.