Mbunge wa Jimbo la Ludewa *Mhe. Joseph Kamonga* alifanya ziara kwenye baadhi ya miradi inayoendelea kutekelezwa ndani ya wilaya ya Ludewa, na kuweza kujionea maendeleo ya miradi hiyo na changamoto wanazo kumbana nazo wakati wa utekelezaji.
Ziara ya Mheshimiwa Mbunge ilihusisha miradi ifuatayo.
*1. Shule ya Sekondari kata ya Lubonde.*
- Utekelezaji wa mradi huu kamati ilipokea kiasi Cha Tsh. 470,000,000 ambazo niza awamu ya kwanza na majengo yanayo takiwa kukamilika kwa fedha hiyo ni,
-Jengo la Utawala ambalo limefika hatua ya kuweka bimu.
- Madarasa nane yapo hatua ya kuweka bimu.
- Maabara 1 ipo hatua ya kuweka bimu.
- Maktaba ipo hatua ya kuweka bimu
- Vyoo vipo hatua ya kusimamisha ukuta
- Maabara mbili zipo hatua ya jamvi.
Licha ya changamoto ndogondogo zinazo wakumba lakin ujenzi unaendelea vizuri na wanachi wanajitoa kwa moyo kuhakikisha ujenzi unakamilika halaka na wanafunzi waanze kusoma.
*2. Shule ya Msingi Kiyombo.*
Ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa na Nyumba pacha ( Nyumba yenye uwezo wa kuchukua familia mbili ) kwaajili ya walimu.
Utekelezaji wa mradi huu upo chini ya mfuko wa TASAF na unagharimu zaidi ya kiasi cha Shilingi milioni 111.
Ujenzi uneendelea vizuri na wanatarajia kumaliza mapema ili vyumba vya madarasa na nyumba ya Mwalimu ikamilike na kuanza kutumika ili kuongeza ufanisi katika shughuli nzima ya utoaji Elimu kwa wanakiyombo.
*3. Ujenzi wa VETA Shaurimoyo.*
Utekelezaji wa mradi huu Serikali imetoa Bilioni 5 na milioni 400 kwaajili ya ukamilishaji wa mradi huu na chuo kianze kutoa hudumu kwa wananchi.
Utekelezaji wa mradi huu unaendelea ijapo kuwa wapo nyuma ya mda kutokana na changamoto mbalimbali zinazo wakabili kama upatikanaji wa umeme wa uhakika na mchanga mzuri unaofaa kwaajili ya utengenezaji wa tofali, kwani malighafi hiyo wanaisafirisha kutoka Mkiu na Makambako.
Mheshimiwa Mbunge kawaasa kuongeza juhudi na ufanisi ili kuhakikisha ujenzi unakamilika mapema iwezekanavyo kwani serikali imeshatoa fedha zote kilichobaki ni utekelezaji wao na kukamilisha ujenzi kwa mdaa walio wekekewa.
*4. Ujenzi wa kituo Cha afya Mundindi*
Utekelezaji wa kituo Cha afya Mundindi Serikali imetoa kiasi Cha Shilingi Milioni 500 kupitia fedha za tozo.
Kutokana na Sensa iliyofanyika mwaka 2012 Tarafa ya Liganga ina jumla ya wananchi 40,000, Hivyo kukamilika kwa kituo hiki Cha afya ambacho kimepewa hadhi ya kituo cha afya cha tarafa kitahudumumia wananchi zaidi ya Elfu 40 ndani ya tarafa.
Maendeleo ya Mradi huu yapo hatua nzuri na Hivyo wananchi wategemee kuanza kupata huduma mapema iwezekanavyo
.
- Jengo la Utawala na OPD lipo hatua za mwisho wanamalizia kupaka rangi ya awam ya pili.
- Jengo la Maabara nalo lipo hatua za mwisho na baadhi ya Vyumba vimekwisha kamilika
- Kizimba cha kuchomea taka kimesha kamilika
- Kwasasa kazi inayoendelea ni kuset msingi wa jengo la huduma ya mama na mtoto na wanaendelea vizuri na tutegeme kuanza kupokea huduma.
*5. Ukaguzi wa barabara ya Muholo - Lugarawa*
Pia Mheshimiwa Mbunge alipata wasaa wa kutembelea ujenzi wa barabara ya Muholo mpaka Lugarawa ambayo inaendelea vizuri na inapitika vizuri Kwasasa.
Barabara hii ilikuwa ina umuhimu mkubwa Sana kwani ilikuwa inaunganisha kata nne za Luana, Ludende, Mkongobaki na Lugarawa, Hivyo kukamilika kwake kutarahisisha usafiri kwa wananchi wa maeneo hayo kwenda makao makuu ya wilaya.
*6. Ukaguzi wa barabara ya Mbwila - Lifuma.*
Barabara hii inaunganisha kata ya Luana Tarafa ya Mawengi na kata ya Lifuma iliyopo Tarafa ya Mwambao.Hadi sasa barabara hiyo imetengewa Kiasi ch milioni 250 na barua ya kuomba fedha zaidi imeishawasilishwa serikalini.
Mpaka sasa Km 1.7 ya barabara hiyo imeshafunguka kuanzia kijiji cha Mbwila.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.