Jana tarehe 15/08/2022 Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Joseph Kamonga alihutubia mikutano miwili kata ya Mavanga Kijiji cha Mavanga na Kijiji cha Mbugani.
Wanakijiji cha Mavanga walitoa shukrani zao za dhati kwa Mheshimiwa Mbunge kwa michango yake ambayo amekuwa akiitoa siku hadi siku na kwa jitihada anazazoendelea kuzionyesha za kupigania maendeleo ya Wanaludewa.
Mhe. Mbunge amechangia Tsh.400,000/= kwaajili ya kutengeneza vitanda kwaajili ya Shule ya sekondari Mavanga. Ikumbukwe awamau ya kwanza Mhe. Mbunge aliweza kuchangia Milioni 1 kwaajili ya vitanda ambavyo vimesha anza kutumika.
Mhe. Mbunge alitoa Milioni moja kwaajili ya kuandalia tofali zitakazo tumika katika ujenzi wa zahanati Kijiji cha Mbugani.
Mhe. Mbunge alimpigia simu Naibu waziri wa maji Mhe.Marryprisca Mahundin aweze kusikiliza kelo ya maji kwa wananchi wa kijiji cha Mbugani ambao hawajakabidhiwa mradi wao. Naibu waziri ameahidi kufanyia kazi Kumalizia mradi huo na kuukabidhi kwa wananchi.
Mhe. Mbunge alikabidhi mipira mitatu kwa vijana kwa matawi matatu ya kata ya Mavanga ambao walimuomba wakati wa mkutano.
Aidha Mheshimiwa Mbunge aliwahamasisha wananchi kujitokeza kwa Wingi kujiandikisha kwenye kitabu cha Mbolea za ruzuku ili waweze kupata kwa bei ya punguzo.
Pia Mhe. Mbunge aliwahamasisha wananchi wote wa kata ya Mavanga kujiandaa kikamilifu kwaajili ya sensa na kutoa ushirikiano kwa maafisa wa sensa watakao pita kwenye kaya zao kukusanya madodoso.
Lakini pia Mhe. Mbunge aliwaasa wananchi wa Mavanga kutouza chakula chote walicho kipata mwaka huu kwakuwa bei ya mazao ni nzuri kawataka wahifadhi ndani chakula cha kuitosha familia zao ndipo kitakacho baki wakiuuze.
Baada ya kumaliza ziara kata ya Mavanga Mhe. Mbunge alipita kukagua ujenzi wa chuo cha ufundi stadi Shaurimoyo (VETA).
Ameridhishwa na Mwenendo wa ujenzi unavyo endelea na kutegemee kuanza kutoa Mafunzo ya mda mfupi siku za hivi karibuni.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.