Jeshia Polisi Wilayani Ludewa limeanzisha mashindano ya Mpira wa miguu yanayokutanisha zaidi ya wananchi 1000 wa Wilaya ya Ludewa lenye lengo la kuwahamasisha wananchi kutojihusisha na vitendo vya kihalifu huku elimu ya Maswala mbalimbali ikitolewa katika uwanja huo ikiwa ni pamoja na elimu ya kutokomeza matumizi ya Madawa ya Kulevya, elimu ya kuanzisha vikundi vya Vijana na kupatiwa elimu ya kupata mikopo ya asilimia kumi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa nk.
Mashindano hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva ambaye ndiye mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano hayo.
Aidha ufunguzi wa mashindano hayo umefanyika Jana Machi 23, 2023 katika Uwanja wa mpira wa miguu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ambapo yanatarajiwa kuwa na fainali Machi 26 siku ya jumapili mwaka huu.
Kwa upande wake Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ludewa SSP Deogratius Massawe amewaambia wananchi wa Wilaya ya Ludewa kuwa kuanzishwa kwa mashindani haya kunawapa chachu vijana kujihusisha na michezo lakini pia kutojihusisha na Uhalifu na matarajio ya kilele cha mashindano hayo zitatolewa zawadi mbalimbali kwa washiriki wote walioshiriki mashindano hayo yaliyopewa jina la POLISI JAMII CUP.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.