Jeshi la Polisi Wilayani Ludewa lilianzisha mashindano ya mpira wa miguu na kukutanisha Vijana wa wilaya ya Ludewa kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kutojihusisha na vitendo vya kihalifu huku wakitoa elimu ya masuala mbalimbali katika uwanja wa mpira wa miguu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Kwa upande wake Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ludewa SSP Deogratius Massawe amewaambia wananchi wa wilaya ya Ludewa kuwa kuanzishwa kwa mashindani hayo kumewapa chachu vijana kujihusisha na michezo lakini pia kutojihusisha na uhalifu.
Sambamba na hayo imetolewa elimu kuhusiana na ukatili wa kijinsia iliyotolewa na mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto wa wilaya ya Ludewa A/INSP Violeth Gideon, elimu ya usalama barabarani husuaani kwa madereva wa bodaboda iliyotolewa na Kaimu DTO wilaya ya Ludewa A/Insp. Naftali Mwinuka pamoja elimu ya kujikinga na majanga ya moto iliyotolewa na Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wilaya ya Ludewa S/SGT Mkingule.
Mashindano hayo yamesimamiwa na Jeshi la Polisi wilaya ya Ludewa na kutolewa zawadi mbalimbali kwa washindi pamoja na timu zote zilizoshiriki ambapo mshindi wa kwanza ni timu kutoka Shule ya sekondari Chief Kidulile waliopata zawadi ya fedha taslimu Tshs. 100,000/- mpira mmoja na jezi. Mshindi wa pili ambao ni Vijana Stars FC kutoka Ludewa Kijijini wamepata zawadi ya fedha taslimu Tshs. 50,000/- mpira na jezi ambapo timu zilizobakia zimepata zawadi ya jezi kwa kila timu.
Aidha ufunguzi wa mashindano hayo ulifanyika Machi 23, 2023 katika uwanja wa mpira wa miguu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na Mgeni rasmi wa ufunguzi wa mashindano hayo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva na leo Machi 26, 2023 ndio hitimisho na fainali ya mashindano hayo.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.