Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe Anthony Mtaka
mara baada ya Makabidhiano ya Ofisi Kati ya yeye na
aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo ambaye ameamishiwa
katika Mkoa wa Songwe ,Mhe.Waziri Kindamba
ameeleza vitu muhimu vya kuanza katika safari ya
ukuu wa Mkoa tangia ateuliwe Kuhudumu Mkoa wa
Njombe
"ni Suala la elimu pamoja na kuinua uchumi
wa Watu, katika suala la Elimu Mkuu wa Mkoa Mhe.
Anthony Mtaka amezitaka shule za Sekondari na
Msingi kuhakikisha wanaongoza katika mitihani ya
kitaifa endapo mikakati aliyoiweka uminafuatwa na
idara ya elimu kwa kushirikiana na Wazazi katika
kusimamia masuala ya elimu".
Aidha akaitaja Mikoa
ambayo Rc Mtaka anaenda kushindana nayo na
kuwaambia wasaau kutajwa kuingoza tena Kitafaifa
badala ni zamu ya Njombe kuingoza Taifa katika
masuala ya elimu.
Katika lengo lake la pili ni kuhakikisha ananyanyua
uchumi wa Watu kwa kuakikisha Halmashauri zote
Mkoani Njombe wanakuwa na vitega uchumi vyao
kwa lengo la kutoa ajira kwa Wananchi pamoja na
kuwakaribisha wawekezaji ambao watakuwa
matokeo chanya kwa Wakazi wa Mkoa wa Njombe.
Ameyazungumza hayo leo katika makabidhiano ya Ofisi katika
ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe wakiwepo
Vongozi mbalimbali wa Dini, Serikali pamoja na
Taasisi
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.