Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa Ndg. Daniel Ngalupela leo tarehe 04 Aprili 2023 ameongoza kikao cha nne cha wajumbe wa Kamati ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Kikao hicho kimehudhuliwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg Ahobokile Songela, Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Ludewa, Viongozi wa Dini pamoja na Wakuu wa Divisheni na Vitengo vya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Pamoja na Mambo mengine Kikao hicho kimejadili maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka2023.
Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 Umewashwa rasmi Mkoani Mtwara na Wilaya ya Ludewa ndiyo Halmashauri ya kwanza katika Halmashauri za Mkoa wa Njombe kuupokea Mwenge wa Uhuru na Mwenge huo utatokea Mkoa wa Ruvuma.
Ujumbe Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 unazingatia umuhimu wa Kuhifadhi Mazingira na kutunza vyanzo vya Maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.