Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva leo tarehe 23 Machi 2023 ameongoza kikao cha tatu cha wajumbe wa Kamati ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Kikao hicho kimehudhuliwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa Bw. Danieli Ngalupela, Muwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Mathan Chalamila, Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Ludewa, Viongozi wa Dini pamoja na Wakuu wa Divisheni na Vitengo vya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Pamoja na Mambo mengine Kikao hicho kimejadili na kuanza maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka
2023.
Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 unatarajiwa kuwashwa rasmi Mkoani Mtwara na Wilaya ya Ludewa ndiyo Halmashauri ya kwanza katika Halmashauri za Mkoa wa Njombe kuupokea Mwenge wa Uhuru na Mwenge huo utatokea Mkoa wa Ruvuma.
Ujumbe Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 unazingatia umuhimu wa Kuhifadhi Mazingira na kutunza vyanzo vya Maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.