Wakati kikao kazi cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kikiendelea Jijini Tanga pamoja na Mambo mengine yanayo jadiliwa kwenye kikao hicho, Maafisa Habari kote nchini wamepata fursa ya kujifunza namna bora ya kutangaza Miradi na vipaumbele vya Serikali, wakati huo Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ametoa wazo la kuanzisha Chaneli ya Runinga ya Maelezo TV kwaajili ya mambo yafuatayo,
1.Uwepo wa chaneli hiyo itarahisisha urushaji wa maudhui (vipindi/matukio/habari) ya Serikali pekee yanayozalishwa kila siku na Maafisa Habari zaidi ya 350 kutoka Wizara, Idara, Taasisi, Mikoa na Wilaya nchi nzima ambayo kwa sasa yanakosa nafasi ya kutosha katika vyombo vya habari.2.
Chaneli hiyo ya Televisheni sio Kituo cha Televisheni, bali Chaneli hii itasaidia kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa bajeti kwa ajili ya kulipia muda wa hewani (Airtime) hali inayosababisha wananchi kukosa taarifa muhimu.3.
Uendeshaji wa chaneli hii utafanywa na Wataalamu waliopo Idara ya Habari (MAELEZO) na hivyo hatutaajiri Watumishi kwa ajili ya Chaneli labda ikiamliwa vinginevyo.
4. Chaneli hii itatatua changamoto ya vituo vya Luninga kulazimika kufuta vipindi vyake pale kunapokuwa na matukio ya kiserikali yanayochukua muda mrefu. Mfano tukio la Serikali linaloanza saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni likirushwa litasababisha Vipindi vingi vya televisheni husika kukosa muda. Hali ambayo husababisha kukatwakatwa kwa matangazo ama vyombo vya habari kupoteza mapato
5. Na nyingine nyingi.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.