Wananchi wa Kata ya Lugarawa Wilayani Ludewa wamejitokeza kwa wingi usiku wa Tarehe 13 Juni, 2022 kutazama Filamu ya The Royal Tour.
Filamu hiyo imeoneshwa katikati ya Soko la Kijiji cha Lugarawa ambapo Viongozi mbalimbali wa Kiserikali walihudhulia kutazama Filamu hiyo.
Akizungumza kwa njia ya Simu Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Andrea Tsere aliwapongeza wananchi wa Lugarawa kujitokeza kwa wingi kutazama Filamu hiyo.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sanday Deogratias alipata nafasi ya kuwasalimia wanachi kwa njia ya Simu walio kusanyika kwa wingi kutazama Filamu ya The Royal Tour.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa aliongea na wananchi na kuwakumbusha umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi itakayo fanyika tarehe 23/08/2022.
Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo Mhe. Erasto Mhagama amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Ludewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa kuwaona wananchi wa Kata hiyo na kuwaletea Filamu ya The Royal Tour.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.