Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan leo anahitimisha maonesho ya nanenane Jijini Mbeya kwa mwaka 2022 Idara ya Kilimo kutoka Wilaya ya Ludewa imeshiriki maonesho hayo kutoka tarehe 31 hadi Leo tarehe 08/08/2022.
Na wananchi wa Wilaya ya Ludewa waishio jijijni Mbeya wamependezwa na uwepo wa maonesho hayo haswa kwa utangazwaji wa fursa ya Kilimo kutoka Wilayani Ludewa.
Kwaupande wao Wajasiriamari wadogo na wazalishaji mbegu mbalimbali kutoka Wilaya ya Ludewa walioshiriki kuonesha mazao yao pale Jijini Mbeya wamempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratias kwa kuuona umuhimu wa kuwashirikisha ili kwenda kutangaza fursa za kilimo nje ya Wilaya ya Ludewa.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.