Na hapa nakusogezea kwa ufupi historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
#Na Chrispin Kalinga.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa tarehe 26 Aprili 1964 ikiwa ni Muungano wa Mataifa mawili huru ya Jamhuri yaTanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo yaliingia mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume mnamo tarehe 22 Aprili 1964 huko Zanzibar.
Mkataba huo ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi hapo tarehe 26 Aprili 1964. Tarehe 27 Aprili 1964 viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam na kubadilishana Hati za Muungano.
Sheria za Muungano zilitoa tamko la Jamhuri ya Muungano katika Ibara ya 4 kwamba: “Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitalazimika, baada ya kuungana na siku zote baada ya kuungana, kuunganishwa kuwa Dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar’ (Ibara ya 4 Sheria za Muungano).
Jina hili la “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar” lilibadilishwa baadaye mnamo tarehe 28 Oktoba 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Sheria ya Jamhuri ya Muungano, namba 61 ya mwaka 1964.
Itakumbukwa tendo ambalo lilifanyika siku hiyo ambapo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar ikiwa ni ishara ya kuunganisha nchi mbili wakati wa Sherehe ya Muungano Dar es Salaa mnamo tarehe 26 Aprili 1964.
"kumekuwa na faida nyingi za kiuchumi kisiasa na kijamii zinazotokana na Muungano wetu, ambazo wananchi wa pande mbili za Muungano wameendelea kunufaika nazo,Mfano wa moja kwa moja ni muingiliano wa kibiashara ambao unaleta faida kiuchumi wa Taifa".
#JastinMlwale
#Mwalimu
"Katika kipindi cha miaka 59 ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar nchi yetu ya Tanzania imepiga hatua kubwa kiuchumi kwa muingiliano wa kibiashara, leo wazanzibar huja bara na wa bara huenda Zanzibar kufuata bidhaa hiyo ni tu ni Mafanikio."
#JastinMlwale
#Mwalimu
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.