Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Gilberth Ngailo leo Juni 06, 2022 amepokea gari moja la TASAF kutoka kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan.
Wakaati akipokea gari hilo amemshukuru Rais kwa kuipa Halmashauri gari hilo litakalo toa adha iliyo kuwepo kwa kuwafikia wananchi kwa wakati na kuwarahisishia TASAF Wilaya ya Ludewa kufanya kazi zao kwa weredi.
Katika hatua hiyo Kaimu Mkurugenzi amewakabidhi TASAF Wilaya ya Ludewa gari hilo na kuwasihi kuendelea kufanya kazi kwa kasi nyingine ukilinganisha na wakati uliopita kwani Rais amewarahisishia kazi kwa kuwaleta gari mpya.
Kwa upande wake Mratibu wa TASAF Wilaya ya Ludewa bwana James Silomba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea gari hilo ambalo litarahisisha utekelezaji wa kazi kwenye Wilaya ya Ludewa.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.