Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kwa Wilaya ya Ludewa linaendelea kwa kasi ikiwa baadhi ya maeneo yanatarajiwa kumalizika kabisa.
Tathimini hiyo imepatikana leo Agosti 25, 2022 wakati kamati ya Sensa ikiendelea na ziara yake ya kutazama maendeleo ya zoezi hilo huku Mjumbe wa Kamati ya Sensa ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratias ambaye pia ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa akiambatana na timu nzima ya Viongozi mbalimbali wametembelea Tarafa ya Mawengi, Tarafa ya Mlangali na Tarafa ya Liganga huku Tarafa ya Masasi ikiwa imengozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ndiye Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Andrea Tsere na Tarafa ya Mwambao tayari ilifikiwa siku ya Jana Agosti 24, 2022.
Kwa Tarafa zote tano za Wilaya ya Ludewa tayari zimefikiwa na kufanikiwa kwa asilimia 95 huku kwaupande wa vitendea kazi hakuna hata kimoja kilicho tolewa taarifa ya upotevu au uharibifu.
Mwenyekiti wa zoezi la sensa ya watu na makazi wilaya ya Ludewa Mhe. Andrea Tsere akiwa katika Tarafa ya Masasi amesema ameridhishwa na mwenendo wa zoezi hilo ambapo ndani ya siku mbili wameweza kuwafikia wananchi kwa asilimia kubwa, hayo ameyasema alipokuwa katika ziara ya kukagua zoezi hilo na kuongeza kuwa watu wamekuwa na mwitikio mzuri.
Sanjali na hilo pia mkuu huyo amewataka makalani wote na wasimamizi kuendelea kutoa elimu kwa watu juu ya zoezi hilo.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.