Mkuu wa Mkoa Wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka leo Desemba16, 2022 amepokea Madarasa 98 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.96 yaliyojengwa katika Mkoa wa Njombe.
Madarasa hayo yote yamekamilika tayari kwaajili ya kupokea Wanafunzi watakaoanza Kidato cha Kwanza Mwezi Januari 2023.
Akizungumza katika Uzinduzi huo Mhe. Anthony Mtaka ameeleza kwamba ameridhishwa na ushirikiano kutoka kwa Wakurugenzi na Wataalamu wengine tangu kuanza hadi kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo.
"Ifikapo Januari 9, 2023 Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanatakiwa kuripoti shuleni bila kujali ana sare au hana, je amelipa ada au hajalipa na nitalifuatilia hili" amesema Mhe. Mtaka.
Aidha amewahimiza Walimu kuwasisitiza wanafunzi kutunza Madarasa hayo na Samani zote zilizopo katika vyumba vya Madarasa hayo.
Mbunge wa Jimbo la Makambako Mhe. Deo Sanga amewasisitiza Wanafunzi kujituma katika masomo kwa kuwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi ili kuhakikisha Wanafunzi wanakuwa na Miundombinu bora.
Uzinduzi huo wa Madarasa umehusisha wilaya ya zote nne zibazounda Mkoa wa Njombe yaani Wilaya ya Njombe, Wanging'ombe, Ludewa na Makete.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.