Zoezi la upimaji wa Udongo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa limeanza na tayari wataalamu kutoka makao makuu ya Wilaya ya Ludewa wameanza kuwahudumia wananchi wanaohitaji kupimiwa udongo mashambani mwao.
ikumbukwe kwamba kipimo cha udongo kwaajili ya kilimo cha mazao ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwakipindi cha miaka yote hakikuwepo na sasa serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wakulima imefanikiwa kuwafikia wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa lengo la kufanya uzalishaji wa mazao yenye tija kwa uhakika.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.