Mapambano dhidi ya UDUMAVU kwa Wilaya ya Ludewa yanaendelea kwa utoaji elimu katika Makundi mbalimbali ikiwemo kwawakina mama wajawazito, walezi nk.
Hapa tunakutana na moja ya mwananchi wa Wilaya ya Ludewa aliweza kutoa maoni yake juu ya uendelezwaji wa kampeni ya TOKOMEZA UDUMAVU, NA LUDEWA BILA UDUMAVU INAWEZEKANA.
Bwana Addy Steven Kalinjila alitoa maoni yake katika grop la WhatsApp kwakubainisha Makundi ya Mlo kamili na kusema kuwa, Labda Tuangalie Makundi ya vyakula na mlo kamili
1. Vyakula vya Protini;
Vyakula vyenye asili ya wanyama: Vyakula vyenye asili ya wanyama ni pamoja na nyama, samaki, dagaa, maziwa, mayai, jibini, maini, figo, senene, nzige, kumbikumbi na wadudu wengine wanaoliwa.
Husaidia mwili kukarabati sehemu zilizo chakaa, kuimarisha kinga ya mwili, kuzuia upungufu wa damu na kuuwezesha mwili kufanya kazi kwa ufanisi.
2. Vyakula vya Wanga
Vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi: Vyakula hivi ndivyo vinavyochukua sehemu kubwa ya mlo na kwa kawaida ndiyo vyakula vikuu. Vyakula katika kundi hili ni pamoja na mahindi, mchele, mtama, ulezi, ngano, uwele, viazi vikuu, viazi vitamu, muhogo, magimbi, viazi mviringo na ndizi.
Huupa mwili nguvu ya kufanya kazi
3. Vyakula vya Vitamini na Madini
Matunda: Kundi hili linajumuisha matunda ya aina zote kama papai, embe, pera, limau, pesheni, nanasi, peasi, chungwa, chenza, zambarau, parachichi, ndizi mbivu, fenesi, stafeli, mabungo, madalansi, pichesi na topetope.
Aidha ikumbukwe kuwa matunda pori au yale ya asili yana ubora sawa na matunda mengine.
Matunda hayo ni kama ubuyu, ukwaju, embe ng’ongo, mavilu na mikoche.
Huupa mwili uwezo wa kuzuia na kupambana na maradhi na kuwezesha mwili kufanya kazi kwa ufanisi. Pia husaidia kulainisha choo
4. Mboga-mboga:
Kundi hili linajumuisha aina zote za mboga-mboga zinazolimwa na zinazoota zenyewe.
Mboga-mboga ni pamoja na mchicha, majani ya maboga, kisamvu, majani ya kunde, matembele, spinachi, mnafu, mchunga. Aina nyingine za mboga-mboga ni pamoja na karoti, pilipili hoho, biringanya, matango, maboga, nyanya chungu, bamia, bitiruti, kabichi na figiri.
Huupa mwili uwezo wa kuzuia na kupambana na maradhi na kuwezesha mwili kufanya kazi kwa ufanisi. Pia husaidia kulainisha choo
5. Vyakula vya mafuta
Mafuta:
Mafuta ni muhimu lakini yanahitajika kwa kiasi kidogo mwilini. Mafuta yanaweza kupatikana kutoka kwenye mimea kama mbegu za alizeti, ufuta, pamba, korosho, karanga na mawese. Mafuta pia yanaweza kupatikana kutoka kwa wanyama, kwa mfano: siagi, samli, nyama iliyonona na baadhi ya samaki.
Huupa mwili nguvu kwa kiasi kikubwa
Maji: Inapaswa kunywa maji safi na salama ya kutosha, angalau lita moja na nusu (au glasi nane) kwa siku ili kuzuia kusaidia maziwa kuzalishwa kwa wingi. Vile vile unaweza kuongeza maji mwilini kwa kunywa vinywaji kama supu, madafu, togwa na juisi halisi za matunda mbalimbali.
Husaidia maziwa kutoka kwa wingi na kuzia upungufu wa maji mwilini. " *Alieleza bwana Kalinjila*
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.