Leo Julai 06, 2022 Kikao cha robo ya nne cha kupinga Ukatili dhidi ya Mtoto na Mwanamke kwa kipindi cha robo ya nne (Aprili hadi Juni 2022) kimefanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kikiongozwa na aliye muwakilisha Mkurugenzi/Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Thomas Kiowi.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimejadili namna bora ya upatikanaji wa taarifa kwa wanafunzi wa shule wa za Msingi na Sekondari.
Akizungumza katka kikao hicho muwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa bwan akiowi amesema kuwa unyanyasaji kwa wanafunzi mashuleni upo na unyanyasaji huo umekosa mahali sahihi kwa kutoa taarifa lakini pia Usalama wa mwanafunzi mtoa Taarifa, kilupitia kikao hiki tuwaombe wanafunzi wote watoe taarifa za Ukatili mashuleni kupitia sanduku za maoni zilizopo katika Shule zote za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Sambamba na hayo shule zote zikiunda tume za wnaafunzi za ufuatiliaji wa taarifa za Ukatili mashuleni zitakazo kuwa zinaripoti.
Aidha katika kikao hicho kumewasilishwa taarifa mbalimbali kutoka kwa wadau wa Ukatili wa kijinsia wakiwemo
1. Kitengo cha Ustawi wa Jamii
2. Polisi Dawati
3. Miso
4. Paralegal
5. Lupao
6. Mahakama
7. Afisa Elimu Msingi
8. Afisa Elimu Sekondari
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.