Afisa Mtendaji wa Kata ya Ludewa Ndg. Alanus Bunda leo Februari 20,2023 ameongoza kikao cha wadau wa Kilimo kilicholenga kutoa elimu kwa vijana na kujishughulisha katika Kilimo cha mbogamboga na matunda.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi mdogo wa kata hiyo huku washiriki wa kikao hicho wakiwa ni vijana waliojitokeza kupata mafunzo ya namna wanavyoweza kujikwamua kiuchumi kwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali zilizopo kwenye mnyororo wa thamani wa mboga na matunda na lishe.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho muwakilishi wa maradi mkuu wa Agri-Connect unaofadhiliwa na Jumuiya ya Nchi za Ulaya kutokea shirika la RIKOLTO Bw. Emmanuel Seni, ambaye pia anawakilisha vituo vitatu atamizi vya ubunifu na kilimo biashara (Agriedo Hub, Kiota Hub na Agrihub) vinavyotekeleza mradi huu wa vijana ujulikanao kama Generation Food Accelerator (GFA) amesema kuwa, Vijana ni nguvu kazi ya Taifa na kwakutambua umuhimu na uhitaji ajira kwa vijana wao Kama shirika wameona wanakila sababu ya kushusha elimu kwa Vijana ya kupambana na wimbi la ukosefu wa ajira na badala yake kupitia Kilimo cha mbogamboga na matunda Vijana wengi watajiajiri na kupata fedha za kutimiza mahitaji yao.
Sambamba na hayo aliongeza kwa kusema kuwa mradi huo unaenda kunufaisha vijana 300 wa mikoa mitano ya Nyanda za juu kusini mwa Tanzania (Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Katavi) ambapo vijana 75 wa Mkoa wa Njombe watanufaika na mradi huo kwa kupatiwa elimu ya ujuzi wa kilimo biashara, ujasiriamali na usimamizi wa fedha kupitia kambi ya mafunzo kwa muda wa wiki moja. Washindi wa mradi huo watapatiwa mitaji ya kuendeleza biashara zao bunifu zinazolenga kutatua changamoto zilizopo kwenye mnyororo wa thamani wa mboga na matunda, ikiwa pamoja na kufungua fursa za ajira na kuajiri vijana wengine.
Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Wilaya ya Ludewa ambaye pia ni msimamizi wa mazao ya bustani na Lishe Wilaya ya Ludewa Bi. Fausta Baha amesema Vijana wa Ludewa wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo kwani ukiondoa kujiingizia kipato mradi huo utanufaisha wananchi wa Wilaya ya Ludewa kupitia ubunifu wao
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.