Sekta ya Kilimo ni mhimili wa uchumi wa Tanzania na imekuwa ikichangia Pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa ujumla pia ni tegemeo la mapato ya fedha za ndani na za nje ya nchi.
Sekta hii imeajiri zaidi ya asilimia 70 ya idadi ya watu wote nchini na kuzalisha mazao ya chakula na biashara.
Mazao makuu ya chakula ya aina ya wanga yanayozalishwa ni pamoja na mahindi, muhogo, mpunga na mtama. Mazao mengine ni ndizi, viazi vitamu na viazi mviringo, ngano, ulezi na uwele.
Mazao ya mikunde ni pamoja na maharage, kunde, mbaazi, choroko na njegere. Mazao yote hayo ndiyo yanayochangia Taifa kujitosheleza kwa chakula kwa zaidi ya asilimia 100.
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imebarikiwa kuwa na ardhi yenye rutuba ya kurutubisha kila mmea unaoteshwa katika ardhi hiyo.
Katika picha ni shamba kubwa la mradi wa Kilimo la Magereza Wilaya ya Ludewa lenye kubwa wa ekari 400.
Mkuu wa gereza la Ludewa SPJoanes Z. Baitange alipokuwa akizungumza na Afisa Habari wa Wilaya ya Ludewa Bw. Chrispin Kalinga alisema kuwa, mpango wa mradi wa Kilimo wa gereza hilo ni kuongeza kasi ya uzalishaji kila mwaka huku akiwasihi vijana kujikita katika kilimo.
Kutoka na maelezo haya Makuu, naomba nitumie nafasi hii kukukaribisha wewe mtanzania kuja kufanya uwekezaji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwenye sekta ya Kilimo cha Mahindi, Maharage, Alizeti,Kahawa, Korosho, Mpunga pamoja na mazao mengine mengi.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.