Mkurugenzi wa Michezo Ofisi ya Rais Tamisemi ambaye pia ni Mratibu wa Mafunzo ya
Mradi wa kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika utunzaji bora wa elimu ya awali
na msingi Tanzania bara (Boost) Ndg. Yusuph Singo amefungua mafunzo ya mradi huo
leo Desemba 16, 2022 yanayoendelea mkoani Iringa.
Mradi huo ambao unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano unalenga kuimarisha
sekta ya elimu nchini hususani katika maswala ya miundombinu.
Wajumbe wa timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ya usimamizi wa mradi wa
BOOST wameshiriki kikao cha kanda leo Desemba 16, 2022 kinachoendelea mkoani
Iringa ambacho kinatarajiwa kuhairishwa kesho Desemba 17, 2022.
Wajumbe hao ni pamoja na Afisa Elimu shule ya Msingi, Afisa Maendeleo ya Jamii,
Mhandisi, Mwalimu Mkuu, Afisa Manunuzi, Mthibiti Ubora wa Shule, Afisa Ustawi wa
Jamii, Afisa Elimu Kata, Afisa Mipango, Afisa Habari na Mratibu wa Mradi.
Pamoja na mambo mengine wajumbe hao wamekumbushwa kuendelea kuhamasisha
uandikishwaji wa wanafunzi wapya wa darasa la awali kwa mwaka 2023 ambapo
waandikishwaji ni watoto wenye umri wa miaka 3-5
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.