Kikao kazi cha wadau wa pembejeo za Kilimo kimefanyika leo Mei 20, 2022 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Akiongoza kikao hicho Afisa Kilimo wa Wilaya ya Ludewa Bi. Clementina Kabaka amesema kuwa, Serikali imejipanga kwa mwaka unao kuja kumrahisishia mkulima kupata pembejeo kwa bei nafuu lakini pia kwa wakati ukilinganisha kwa kipindi kilicho pita.
Aidha akaongeza kwa kusema kuwa lengo kubwa la kikao hicho ni kuboresha huduma za Kilimo ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa Viwatilifu, Mbolea na Pembejeo.
Kikao hicho kimehudhuliwa na makampuni tofauti ikiwemo na Kampuni ya Mtewele General Traders, Kiboseed co. Ltd, Yara Tanzania Ltd na Meru Agro
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.