Leo Julai 06, 2022 Kikao cha Utoaji wa taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za kupinga Ukatili dhidi ya Mtoto na Mwanamke kwa kipindi cha robo ya nne (Aprili hadi Juni 2022) kinaendelea muda huu katika ukumbi wa H/W/Ludewa kikiongozwa na aliye muwakilisha M/M/H/Ludewa Bw. Thomas Kiowi.
Na moja ya mambo yanayo jadiliwa muda huu ni pamoja na namna bora ya upatikanaji wa taarifa kwa wanafunzi zinazo husiana na unyanyasaji kwa wanafunzi mashuleni lakini pia uundwaji wa tume mashuleni zitakazo kuwa zinaripoti Taarifa za Ukatili mashuleni.
Aidha kumewasilishwa taarifa mbalimbali kutoka kwa wadau wa Ukatili wa kijinsia wakiwemo
1. Kitengo cha Ustawi wa Jamii
2. Polisi Dawati
3. Miso
4. Paralegal
5. Lupao
6. Mahakama
7. Afisa Elimu Msingi
8. Afisa Elimu Sekondari
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.