Kikao cha nne cha sherehe za Mbio za Mwenge wa Uhuru kinaendelea leo Machi 17, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na Mwenyekiti wa kikao hicho akiwa ni Kaimu DAS Bw.Linus Malamba akimuwakilisha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere na katibu wa kikao hicho akiwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Gilbart Ngailo akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratias.
Moja ya mambo yanayo jadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na Mapitio ya bajeti za kamati mbalimbali za sherehe za Mbio za Mwenge wa uhuru 2020.
Aidha wajumbe mbalimbali wamehudhulia kikao hicho ikiwemo kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ludewa,Viongozi wa madhehebu ya dini,Viongozi wa Chama cha cha Mapinduzi (CCM) Mwenyekiti wa wafanya biashara,Wazee maarufu pamoja na wadau wengine.
Ikumbukwe kwamba Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2022 unatarajiwa kuwashwa rasmi tarehe 02 Aprili 2022 katika Mkoa wa Njombe ndani ya Uwanja wa Sabasaba Njombe na kwa Wilaya ya Ludewa tunatarajia kuupokea Mwenge huo Tarehe 07 Aprili 2022
Aidha Mwenge wa Uhuru kwa siku hiyo ya Aprili 7, 2022 utakesha Manda na Tarehe 08 Aprili 2022 utakabidhiwa Mkoa wa Ruvuma daraja la mto Ruhuhu.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.