Na. Chrispin Kalinga
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva akiwakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa Ndg. Gilbert Ezekiel sandagila ameongoza kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Wilaya kwaajili ya kuwasilisha na kujadili utekelezaji wa Mradi endelevu wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (SRWSSP) pamoja na kampeni ya usafi wa mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Kikao hicho kimefanyika Leo Oktoba 10, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kikihudhuriwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo baadhi ya wakuu wa divisheni na Vitengo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratias akiwakilishwa na Castor Kibasa, lakini pia kikao hicho kimehudhuriwa na Viongozo wa dini.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimewasilisha mpango mkakati wa utoaji elimu kwa wananchi wa uboreshaji wa miundombinu ya Maji na usafi wa mazingira katika vituo vya kutolea huduma za Afya na shule za Msingi zilizopo Wilayani Ludewa, Uboreshaji wa vyoo bora kwenye kaya na Taasisi zote zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa pamoja na Uboreshaji na uimarishaji wa usafi wa mazingira katika kaya na Taasisi zote.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.