Upatikanaji wa mbegu bora ndio msingi wa kuongeza mafanikio ya uzalishaji mbegu kulingana na mifumo iliyopo ya mbegu kwa mazao mahususi, kuzidisha mbegu kunaweza kufanywa na wabia wa umma au wa sekta binafsi.
Leo Septemba 22, 2022 Kikao cha wadau wa mbegu kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kikiwahusisha wazalishaji wote wa mbegu wa Wilaya ya Ludewa wanaozalisha mbegu za Mahindi, Maharage, Korosho, Kahawa, Mboga mboga nk.
Katika kikao hicho wamejadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwasilisha rasimu ya mwongozo wa jukwaa la mbegu la Wilaya ya Ludewa.
Kikao hicho kimeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Bi. Clementina Kabaka ambaye pia ni Afisa Kilimo wa Wilaya ya Ludewa na kuwezeshwa na SAGCOT
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.